JOSE MOURINHO AENDELEA KUMNYATIA ROMELU LUKAKU

KOCHA Jose Mourinho bado hajakata tamaa ya kupata saini ya straika wa timu ya Everton, Romelu Lukaku na sasa amemweka tena katika orodha ya wachezaji anaowawinda katika orodha ya wachezaji wa dirisha la usajili wa majira ya kiangazi.

Lukaku yupo katika kiwango kizuri kwa hivi sasa na Mourinho amemweka katika rada ya usajili wa majira ya joto.

Akinukuliwa Mourinho alimzungumzia Lukaku kama mchezaji anayeweza kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji.

Mourinho amesema Lukaku ni mtu sahihi wa kuongezwa katika safu ya ushambuliaji ya kikosi chake.

“Ni mmoja wa washambuliaji ninawaona wana kiwango cha kuitumikia United sina mashaka katika azma yangu hii na ndio maana ninapambana kwa ajili ya kupata saini yake.”


Katika kuhakikisha anaweza kumnasa Mourinho aliwatuma mawakala kufuatilia kiwango cha Lukaku katika kila mechi za sasa ili atue Old Trafford ambapo anaweza kucheza sambamba na Ibrahimovic na Paul Pogba.

No comments