JOSE MOURINHO ASEMA WACHEZAJI WABINAFSI LEICESTER WAMEMSALITI RANIERI

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amewashutumu wachezaji wa Leicester City kwa kuwa na ubinafsi wa kumsaliti aliyekuwa kocha wao, Claudio Ranieri.

Mreno huyo alivaa kofia yenye nembo za “CR” akimuunga mkono Ranieri kabla ya kuwashutumu wachezaji hao ambao wengi wao walisaini mikataba mipya baada ya kushinda taji la Ligi.

Mourinho alifutwa kazi katika mazingira kama hayo msimu uliopita kufuatia mgomo wa wachezaji, lakini akasema kuwa kisa alichofanyiwa kilikuwa kidogo sana ikilinganishwa na vile Ranierio alivyofanyiwa.

“Nadhani msimu huu ulianza na ubinafsi mwingi wachezaji wakitaka kupewa mikataba mipya.”

“Watu wakifikiria fedha zaidi wengine wakiamua kuondoka bila kujali ni nani aliyewafanya kufika walivyo,” alisema Mourinho.

Mourinho aliongeza kusema kwamba wachezaji wengi mara zote wamekuwa wabinafsi kiasi kwamba wanachangia makocha kuonekana sio watu wa muhimu wakati kumbe ndio chachu ya mafanikio ya klabu.

“Ukiangalia kilichonitokea mimi pale Chelsea kinaweza kulingana kabisa na kile kilichomtokea Ranieri, kwasababu haiwezekani kocha awape ubingwa leo hii mumuone hafai.”

“Wachezaji wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kuhakikisha Ranieri anatupiwa virago nah ii ni tabia ya kawaida sana katika klabu nyingi za Ulaya, kwa hakika kabisa hali hii haikubaliki.”


Ranieri baada ya kuipandisha Ligi Kuu Leicester aliifanikisha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza na kuiwezesha kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza msimu huu.

No comments