JOSE MOURINHO AWATOLEA "MACHAFU" CONTE, JURGEN KLOPP

HATA kama huna nafasi ya kutafsiri kila kinachosemwa, lakini wakati kauli inapotoka kwa mtu ambaye huwa ana staha lazima uanze kufikiria mengine.

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho kila anapotoa kauli yake amekuwa akitengenezewa tafsiri na wakati mwingine kuambulia lawama.

Kauli yake ya kuwashutumu makocha wenzake kwamba wanadharau michuano ya FA imezaa lawama kwamba kocha huyo anawatukana wenzake.

Vyombo vya habari vya Uingereza tayari vimeanza kumpa lawama kocha huyo kwamba anawatukana wenzake na kwamba kama angekuwa muungwana zaidi alitakiwa kuwaomba radhi kwasababu kila kocha na mipango yake.

Majuzi Mourinho amewashutumu makocha wengine wa kigeni Antonio Conte, Jurgen Klopp na Arsene Wenger kwa kile alichosema kwamba wanaikosea heshima michuano hiyo.

Kocha huyo raia wa Ureno amesema kwamba yeye anaiheshimu sana michuano ya FA na ndio maana huwa anapanga kikosi kinachocheza pia Ligi Kuu tofauti na makocha wenzake ambao mara nyingi hupanga kikosi dhaifu.


Mourinho amekiri kwamba kudharau michuano hiyo ndio sababu ya baadhi ya timu kubwa ikiwemo Liverpool na Southampton kuondolewa katika michuano hiyo.

No comments