Habari

JURGEN KLOPP SASA AKIRI TIMU YAKE INAANGUSHWA NA MAKIPA “NYANYA”

on

AWALI
zilikuwa ni kelele za mashabiki wa Liverpool tu kwamba kikosi chao ni bora
lakini kina makipa wa “kawaida” sana.
Kocha Jurgen
Klopp hakufanya uamuzi wowote wa kusajili kipa wa kutisha katika Ligi Kuu
inayoendelea nchini humo na sasa Liverpool imekuwa na makipa ambao wanaitwa “mashati”
wakiwa golini.
Lakini juzi
tu Klopp mwenyewe amekubaliana na madai ya mashabiki kwamba makipa wa timu hiyo
ndio mchawi mkubwa wa matokeo mabovu.
Wiki iliyopita
Liverpool ilipokea kipigo kutoka kwa Hull City na kudidimiza ndoto zao za
ubingwa huku uwezekano wao wa kubaki kwenye nne bora nao ukiwa mdogo tofauti na
mwanzo.
Klopp amewataja
Simon Mignolet na Loris Karius magolikipa wa timu hiyo kwamba ndio chanzo cha
matokeo yasiyoeleweka ndani ya Livelpool.
Mwanzoni Klopp
alikuwa akimuaminia na kumtumia Mignolet lakini baadae kiwango chake kilionekana
kushuka ghafla na kufungwa mabao ya kizembe.
Faulo iliyofungwa
kwenye mechi dhidi ya Chelsea ilipunguza imani ya Klopp kwa Mignolet ambaye
aliamua kumpa nafasi Karius lakini nae anaonekana kuwa mbovu.
Ikumbukwe mwaka
jana Klopp aliingia katika majibizano na mchambuzi Garry Neville baada ya
Neville kusema Klopp hana uchaguzi mzuri wa makipa.
Baada ya
mechi ya Hull City aliulizwa kuhusu kipa wake na Klopp alisema: “Hilo ni tatizo
letu kwa sasa na linatupa shida, sawa uwanjani hakuwa peke yake lakini unaweza
kuona anavyokosa umakini, tuna tatizo golini kwetu.”
Kocha huyo
raia wa Ujerumani amesema kuwa anajua kwamba mashabiki wa Liverpool
wanamwamini, lakini pia hawawezi kuendelea kuwa na imani nae kama timu
inafungwa kizembe.

“Mimi ni
kocha lazima kila mmoja anipende kwa kazi nzuri, watu wakisema wananipenda bado
katika kazi mbaya itakuwa ni kituko. Lakini lazima niseme kwamba makipa wangu
ni matatizo,” amesema wazi kocha huyo.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *