KHADIJA KOPA, MWANAHAWA ALI JUKWAA MOJA VALENTINE DAY

MALKIA wa mipasho, Khadija Kopa Valentine Day hii anatarajiwa kukutana jukwaa moja na gwiji mwenzie, Mwanahawa Ali ndani ya Darlive, Mbagala jijini Dar es Salaam, imefahamika.

Taarifa kutoka ndani ya Darlive zinasema kwamba magwiji hao watapanda jukwaani siku hiyo huku wakisindikizwa na bendi zao za East African Melody (Mwanahawa Ali) na Tanzania One Theatre (TOT) kwa upande wa Khadija Kopa.

“Shoo hiyo ambayo itaanza kurindima majira ya saa 2:30 usiku, itapambwa na burudani kutoka kwa wasanii kemkemu kama vile; Mc Dalada, Topito na Makhirikhiri wa Bongo,” imesema taarifa hiyo.


Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa, kiingilio kimepangwa kuwa ni sh. 5,000 ambapo zawadi kibao zimeandaliwa kwa mashabiki na wapenzi watakaokuja wawili wawili, wamependeza zaidi ama kucheza kwa kuvutia.

No comments