KHALID CHOKORAA AKIRI KUWA MUZIKI WA DANSI UMEFUNIKIWA NA BONGO FLEVA, SINGELI NA TAARAB


Mwimbaji nyota wa muziki wa dansi Khalid Chokoraa amekiri kuwa dansi limeporomoka na sasa linashika namba nne.

Akiongea katika mahojiano na kipindi cha Lete Raha cha Capital Radio mchana huu, Chokoraa akasema muziki namba moja ni bongo fleva, kisha singeli, taarab halafu ndo unafuta muziki wa dansi.

Mwimbaji huyo wa Twanga Pepeta alikuwa akifafanua ni kwanini ameamua kupiga muziki wa vionjo vya singeli ambapo alisema aina hiyo ya muziki kwa sasa ipo juu kulinganisha na dansi.

“Kibiashara muziki wa singeli ni wa pili, wa kwanza ni bongo fleva, wa tatu taarab halafu ndiyo dansi”, alifafanua Chokoraa.

No comments