KIPA IKER CASILLAS ATAJA CHANZO CHA KUFUNGWA NA JUVENTUS

MLINDA mlango wa FC Porto, Iker Casillas amesema kuwa kadi nyekundu aliyopewa beki wao, Alex Telles ndio iliyosababisha waambulie kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Juventus katika mchezo wa Ligi ya mabingwa.

Katika mchezo huo uliopigwa mwanzoni mwa wiki hii katika uwanja wa Stadio do Dragao beki huyo alitolewa nje kipindi cha kwanza kwa kufanya mak0sa mara mbili.

Kutokana na kutolewa kwa beki huyo, kuliifanya Juventus kutawala mchezo na mabao hayo yaliyofungwa na wachezaji Marko Pijaca na Dani Alves kipindi cha pili kunaifanya timu hiyo kuwa na kibarua kikubwa wakati timu hizo zitakaporudiana mjini Turin.

“Kwa kucheza dhidi ya timu kama Juventus ikiwa na wachezaji wote 11 na nyie mkiwa na 10, ni kazi kubwa,” alisema staa huyo.  


“Mchezo ulibadilika kabisa baada ya beki wetu kutolewa nje licha ya kuwa tulijaribu kutengeneza nafasi nyingi na kuongeza kasi, lakini tulipoteza kabisa mwelekeo,” aliongeza Casillas.

No comments