KIPA WA VIETNAM AFUNGIWA KWA KUPIGWA MABAO KIZEMBE UWANJANI

MLINDA mlango wa timu ya Vietnam, Thanhtoan amepigwa marufuku kucheza soka kwa miaka miwili kwa kuongoza ule unaoitwa mgomo mgando wakati wa mechi.

Pamoja na wachezaji wa timu yake walisimama bila kutingishika hata kidogo wakitazama timu pinzani Ho Chi Minh City kuifunga mabao matatu ya dakika za lala salama kabla ya mechi kukamilika.

Walikuwa wakipinga uamuzi wa refa kuipatia timu hiyo penati iliyokumbana na utata.

Mojawapo ya mabao mengine mawiuli yaliyofuata aliyakwepa hasa kwa kuruka kando kwa makusudi.


Shirikisho la kandanda la Vietnam limempiga marufuku miaka miwili pia nahodha wa timu hiyo likisema mgomo huo ulionyesha utovu wa nidhamu kwa refa.

No comments