KITU CHA “MKWANJA” CHALETA KIZAZAA TIMU YA TAIFA CAMEROON

SAKATA la posho limeendelea kuitesa timu ya taifa ya Cameroon baada ya Jumatatu wachezaji wake kugomea kufanya mazoezi kwa sababu hawajalipwa posho zao.

Vijana hao wa the “Indomitable Lions” wanakabiliwa na kibarua kizito cha mechi ya nusu fainali dhidi ya Ghana itakayopigwa leo Alhamisi.

Licha ya kucheza vyema hadi kuiondoa Senegal kwa penati 5-4 katika robo fainali, viongozi wa chama cha soka Cameroon wangali wanawasumbua kuwalipa posho zao.

Kocha wa timu hiyo, Hugo Broos amewataka viongozi wa chama cha soka kuwalipa wachezaji wao fedha isiyopungua faranga mil 12.


Akizungumzia suala la kugoma kufanya mazoezi, nahodha wa Cameroon, Benjamin Moukandjo amesema hali ikiendelea kuachwa namna hii, wasitarajie ushindi.

No comments