KIUNGO ADAM LALLANA APINGANA NA KLOPP KUHUSU "MCHAWI" WA LIVERPOOL LIGI KUU ENGLAND

WAKATI kocha wa timu ya soka ya Liverpool, Jurgen Klopp akisema kwamba katika kikosi chake kuna wachawi wawili, maana ya makipa wake, mmoja wa wachezaji muhimu katika timu hiyo nae amekuja na yake.

Kiungo wa timu hiyo, Adam Lallana amesema kuwa kukosekana kwa mambo muhimu ya ziada ya kiuzoefu katika timu yao wakiwa hawapo vyema, ndio sababu na changamoto ya azma yao ya kutwaa ubingwa England.

Kauli hiyo imekuja baada ya hivi karibuni Liverpool kushindwa kufanya vizuri dhidi ya Hull City na kutupwa nafasi ya tano kwenye Ligi Kuu England wakiwa na alama 13 nyuma ya vinara Chelsea.

Liverpool chini ya meneja Mjerumani, Klopp, hawajashinda hata mechi moja ya Ligi Kuu mwaka huu 2017 na kutupwa nje ya 4 Bora kwa mara ya kwanza tangu Septemba 24.

Kabla ya mechi ya Hull City, Liverpool wakiwa nyumbani Anfield walitoka sare na Chelsea na hilo lilitegemewa kuwafanya wageuke na kuanza kupata ushindi lakini hali ikawa ni tofauti na mategemeo.

Kipigo toka kwa Hull City kimeendeleza mwenendo wao wa kufungwa na timu “dhaifu” kama vile walivyofanywa msimu huu na timu na timu zilizo nafasi za tisa za mwisho ambazo ni Burnley, Bournemouth, Swansea City na hiyo Hull City.

Lakini Lallana amesema kuwa kukosekana kwa umakini na uzoefu kwa baadhi ya wachezaji kumeifanya Liverpool ionekane kama timu ya kawaida sana katika Ligi Kuu.


“Kuna mambo yanakwenda ovyo. Kuna umakini mdogo kwenye baadhi ya nafasi na unaona kuna watu hawana uzoefu wa kutosha wa kuamua ushindi,” amesema.

No comments