KOCHA ANTONIO CONTE ASEMA PEDRO RODRIGUEZ AMEZALIWA UPYA CHELSEA

INGAWAJE Pedro Rodriguez hakuwa amepewa nafasi ya kung’ara katika msimu huu wa Ligi, lakini sasa anaonekana kama anataka kuwaumbua wale waliokuwa wanamwona kama mchezaji wa kawaida tu.

Nyota huyo wa timu ya Chelsea sasa ameonyesha uhalisia wake na kurejesha makali yake aliyokuwa nayo wakati akiwa katika kikosi cha FC Barcelona.

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amesema kwa nyota huyo amebadilika sana na anaonyesha kazi ambayo ilikuwa imejificha kwenye miguu yake.

Kocha huyo amesema kuwa ni kweli kwamba kuna wakati Pedro Rodriguez alikuwa haonyeshi kama ana msaada mkubwa kwa timu lakini akasema kwamba wachezaji wengi wako hivyo.

Kuna watu walikuwa wanamshangaa kwamba mbona hana ule moto wake ambao alikuwa anauonyesha Barcelona? 
Wengine wakafika mbali na kusema kwamba ingefaa kama angetolewa kwa mkopo. Lakini nilikaa nae nikamweleza kwamba yuko katika Chelsea kuonyesha thamani yake na si vinginevyo. Nadhani sasa mnaiona tofauti,” alisema Conte.


Alipokuwa katika kikosi cha Barcelona alikuwa mwiba mkali kwa staili yake ya kuhama kutoka katika winga moja kwenda nyingine huku akilazimisha mabao katika mazingira magumu.

No comments