KOCHA PEP GUARDIOLA AKIRI MASHABIKI WANAWAPA WAKATI MGUMU

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola anataka wachezaji wake wahimili matarajio yaliyoko mbele yao licha ya kuwa kuna changamoto nyingi kutoka kwa mashabiki.

Meneja huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich amesema kwamba kufundisha timu za Uingereza kunahitaji kuwa na moyo wa chuma kwasababu kuna mashabiki wasiovumilia kushindwa.

“Nimekuwa nikiongea na wachezaji wangu kwamba kila tunapopata matokeo mazuri tunatakiwa tuyatafakari matokeo mabaya pia ambayo mashabiki hawataki kuyasikia,” amesema.

Amesema hata hatua ambayo wamefikia katika Ligi ya Mabingwa Ulaya ni kwasababu wamevumilia tu, ingawa anakiri kwamba katika soka kuna matokeo ya kuudhi pia.

“Watu wanaweza kufikiria Manchester City wanastahili kuwa hapa lakini klabu nyingi kubwa hazijafika hapa, tulipofikia panatokana na uvumilivu ingawa soka linaudhi wakati mwingine,” amesema Guardiola mwenye umri wa miaka 46.


Historia ya hivi majuzi ni nzuri lakini katika historia ya muda mrefu “Manchester City haijakuwa katika nafasi hii kwa muda mrefu, mashabiki wanatakiwa kutuvumilia,” amesema.

No comments