KOCHA WA ARGENTINA AMTETEA MESSI KUSHINDWA KUSHANGILIA BAO ALILOFUNGA DHIDI YA LEGANES

KOCHA wa timu ya taifa ya Argentina, Edgardo Bauza amesema kuwa anavyoamini hasira alizonazo za kulaumiwa straika Messi ndicho kilichomfanya ashindwe kushangilia bao lake alilofunga dhidi ya timu ya Leganes.

Messi ndiye aliyehitimisha bao la ushindi kwa njia ya penati ambalo lilifanya washuhudiwe Barcelona Jumapili wakiondoka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi ya Laliga.

Hata hivyo pamoja na staa huyo wa timu ya taifa ya Argentina kushindwa kushangilia bao hilo na wachezaji wenzake pamoja na makocha wake Luis Enrique ambao waliluka kwa shangwe.

Kutokana na hali hiyo kocha huyo wa timu ya taifa Bauza anasema ni kama kujibu shutuma ambazo Messi alizipokea baada ya kuchapwa 4-0 na PSG katika mechi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Nadhani alikuwa akilipiza lawama alizotupiwa baada ya kufungwa na PSG,” kocha huyo alikiambia kipindi cha redio joga.


“Nilimgundua lama alikuwa ana asaila wakatia lipo funga bao lake,” aliongeza kocha huyo.

No comments