KOCHA WA BURKINA FASO ASEMA HANA "PRESHA" NA MISRI LEO

KOCHA wa Burkina Farso, Paulo Duarte amesema hawana presha na Misri wanayovaana nayo leo kwenye nusu fainali ya Kombe la Mataifa Afrika.

“Tumejiandaa kushinda mchezo huu na ninaamini tuko vizuri,” alisema Duarte.

Duarte alisema nia yao ni kufika tena fainali kama walivyofanya mwaka 2013 nchini Afrika Kusini.


Kocha huyo alikiri haitakuwa kazi rahisi ikizingatiwa Misri ina uzoefu mkubwa na mashindano haya.

No comments