Habari

KOCHA WA SWANSEA NDIO KOCHA BORA WA LIGI KUU ENGLAND MWEZI JANUARI

on

CHAMA cha soka cha Uingereza (FA), kimemtangaza kocha wa Swansea, Paul
Clement kama kocha bora wa Ligi Kuu mwezi Januari.
Ushindi wa timu yake dhidi ya Crystal Palace na Liverpool iliyokufa katika
uwanja wake wa Anfield, ni baadhi ya sababu zilizomfanya kocha huyo awapiku
makocha wengine wote.
Yeye mwenyewe amesema kwamba ameshangazwa na tuzo hiyo, lakini kwake ni sifa
na ufahari mkubwa na kwa kikosi chake.
“Nimeshangazwa na ushindi huu na hapa ndipo unaona kwamba FA wamekuwa
wakiangalia vigezo sahihi. Kwangu mimi ni fahari kubwa na kwa timu yangu,”
amesema Clement.
Amesema kwamba kama mtu angekuwa anaangalia rekodi, pengine labda kocha bora
angekuwa Jose Mourinho wa Manchester United kwa kushinda mechi nyingi, lakini
mwingine angesema kwamba labda Antonio Conte ambaye timu yake ya Chelsea
inaongoza angestahili.
“Najua kwamba wachezaji wangu wanafanya kazi vyema na huu ni ushindi mkubwa
kwetu. Tumekuwa waadilifu katika mechi za nyumbani na ugenini na tunacheza kwa
nidhamu ya hali ya juu. Kila anayeitazama timu yetu anaona uhalisia huo,”
amesema.

Kocha huyo amesema kwamba hatabweteka na ushindi huo na anataka kuona
kwamba Swansea pia inakuwa timu bora katika Ligi Kuu England.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *