KOCHA WA TIMU YA TAIFA CAMEROON AFURAHISHWA NA KIKOSI CHAKE

KOCHA wa timu ya taifa ya Cameroon, HugoBroos amefurahi kikosi chake kuwa familia moja kwa jinsi walivyopigana hatua kwa hatua kunyakua ubingwa wa Mataifa ya Afrika (AFCON).

Michuano ya AFCON ilimalizika nchini Gabon Jumapili iliyopita ambapo Cameroon ilifanikiwa kuwa mabingwa kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Misri.

Cameroon ilipambana kuibukia na ushindi huo katika mchezo mgumu na hivyo kunyakua taji hilo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 15.

“Sina wachezaji 23 kwenye timu yangu, nina marafiki 23,” alisema Broos alipozungumza na BBC.

“Zaidi ya wiki tumetoka kuwa kikosi cha timu na badala yake sisi ni familia moja.”


“Ni jambo ambalo halikutegemewa jinsi vijana walivyofanya. Ni heshima kubwa,” alisema kocha huyo.

No comments