LEICESTER CITY WAKANUSHA KUACHANA NA KOCHA CLAUDIO RANIERI

KLABU ya Leiecester City kwa mara nyingine wamekanusha taarifa za kwamba wanataka kuachana na kocha wao wa sasa Claudio Ranieri.

Badala yake wamesisitiza kuwa wataheshimu mkataba walioingia na mkufunzi huyo ambao utafikia tamati mwishoni mwa msimu wa mwaka 2020.

Hatua ya Leicester City kuweka bayana jambo hili inatokana na taarifa za mitandao zinazovumishwa kwamba klabu hiyo imo mbioni kutaka kuvunja mkataba wa Ranieri ifikapo mwishoni mwa msimu huu.

Kwa mujibu wa taarifa hizo mabingwa hao wa premier msimu wa 2016/17 hawaridhishwi na na mwenendo wa timu hiyo msimu huu chini ya kocha huyo.


“Bado tuna imani na meneja huyu kwa miaka mingine minne kwa ajili ya mafanikio ya "the Foxes" hadi Juni 2020”.

No comments