LEICESTER CITY YASAKA HUDUMA YA MBRAZIL WA HAMBURG

HUKU wakiwa katika hali mbaya msimu huu, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya soka nchini England, Leicester City sasa wameanza kusaka watu wa kuirejesha kwenye makali.

Ni katika madhumuni hayo, mabingwa hao waliopoteza matumanini wanasaka saini ya nyota wa Brazil na timu ya Hamburg FC ya Ujerumani, Walace Souza Silva.

Leicester City imevutiwa na Walace kwasababu aliisaidia sana pia timu yake ya taifa ya Brazil katika kikosi kilichoshiriki Olimpiki na kwa nafasi yake ya kiungo, anaweza kuwa tiba ya tatizo katika timu hiyo.

“Tumesaka mtu sahihi katika kiungo wakati wa dirisha la usajili ni kama hatukupata, lakini pia tumevutiwa sana na Walace tunadhani atatusaidia sana,” amesema mmoja wa maofisa hao.

Lakini pia nyota huyo anasakwa kwa udi na uvumba na timu nyingine ya England, klabu ya Everton.

Kiungo huyo mkabaji mwenye umri wa miaka 21 anatajwa kwamba anataka kuondoka Hamburg na kusaka maisha mapya katika Ligi Kuu ya England ambayo imekuwa na msisimko zaidi.

Lakini kwa mujibu wa gazeti la Mirror, Hamburg iko tayari kuachana nae katika majira ya joto kama tu itakuwa imepata mbadala wake.

No comments