LINAH KUFUNGUA MWAKA 2017 NA KIBAO "KOSA SINA"

BAADA ya kutamba na nyimbo mbalimbali ukiwemo wa “Raha Jipe Mwenyewe”, msanii wa muziki wa bongofleva, Linah Sanga amesema kuwa anaanza mwaka huu 2017 kwa wimbo wa “Kosa Sina”.

Alisema kuwa amekuja kuongeza burudani kupitia wimbo wake huo ambao video imefanywa na mwongozaji Mtanzania Khalfani Khalmandro na imeanza kurushwa kwenye mitandao ya kijamii.


“Nimeanza mwaka 2017 kwa wimbo “Kosa Sina” ambao umeandaliwa katika ubora wa hali ya juu na nina uhakika kwamba wale ambao wameshaiona video ya wimbo huu watakubali kile ninachokisema,” alisema Linah.

No comments