Habari

LIVERPOOL, TOTTENHAM ZAINGIA VITANI KUUWANIA “MTAMBO WA MABAO” WA LIVER PLATE

on

LIVERPOOL ya
Jurgen Klopp imeingia katika kupigana vikumbo na Tottenham na kujikuta wote
wakiwania saini ya mfumania nyavu wa timu ya Liver Plate, Lucas Alario.
Alario yuko
katika kiwango cha juu cha soka kiasi cha kuwaingiza vitani klabu hizo vigogo
wa Ligi yap rimier.
Straika huyo
mwenye umri wa miaka 24, kwa sasa ni kati ya wachezaji wa timu ya taifa ya
wakubwa nchini kwao Argentina.
Hatua ya
kuitwa kwake kucheza sambamba na Lionel Messi kumempa heshima ya hali ya juu ya
kisoka na sasa anawindwa na timu, zikiwemo Liverpool na Spur.
Liverpool wameweka
mezani ofa ya pauni mil 12, ingawa klabu ya Liver Plate imebainisha dau la
kuuzwa kwa Alario ni pauni mil 15.2.
Kwa mujibu
wa jarida la The Sun, azma  ya kocha
Jurgen Klopp amevutiwa na straika huyo lakini hata hivyo ameweka mezani ofa ya
pauni mil 8.5, fedha ambayo Liver Plate wanaikataa.

Pamoja na
Liverpool na Spur pia timu za Inter Milan na Torino za nchini Italia zimo
katika mawindo ya saini ya Alario.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *