LUCAS DIGNE AIFANANISHA BARCELONA NA DINI YENYE WAUMINI WENGI DUNIANI

BEKI wa kulia wa Barcelona, Lucas Digne amefananisha uamuzi wa kuichezea klabu hiyo kama imani ambayo mtu anaweza kuiamini kwa kujiunga na dini kubwa.

“Barcelona ni klabu kubwa hapa duniani, kuamua kuichezea ni kama kuamini dini nyingine kubwa. Klabu hii ina mashabiki wengi duniani kuliko hata baadhi ya waumini wa madhehebu,” amesema.

Kinda huyo wa umri wa miaka 23, amehamia Camp Nou akitokea kwa matajiri wengine wa Paris Saint-Germain kwa uhamisho wa euro mil 16.5 baada ya kusota kwa mkopo katika klabu ya AS Roma.


“Kwangu mimi Barcelona ni klabu kubwa hapa duniani na imani yangu inanituma niifananishe na dini ambayo watu wengi wanaipenda,” alisisitiza Digne.

No comments