LUCAS PEREZ ASEMA WENGER HANA DALILI YOYOTE YA KUFUNGASHA VIRAGO ARSENAL

STAA Lucas Perez amesema kuwa kocha wake Arsene Wenger haonekani kuwa na dalili za kuitema Arsenal ufikapo mwishoni mwa msimu huu.

Kwa sasa Gunners wamerejea katika njia ya ushindi baada ya Jumatatu kushinda 2-0 dhidi ya Sotton United katika mchezo wa Kombe la FA.

Katika mchezo huo Perez ni mfungaji wa bao la kwanza kabla ya Theo Walcott kufunga la pili likiwa ni la 100 kuifungia Arsenal.

Ushindi huo ulikuwa ni mtamu kwa Arsenal na Wenger ambaye ilikuwa ni mechi yake ya kwanza tangu alipofungwa mabao 5-1 na Bayern Munch katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Kutokana na kipigo hicho ziliibuka lawama kubwa kwa Wenger na huku mashabiki wengi wakimtaka afungashe baada ya kuiongoza timu hiyo kwa muda wa miaka 20.

“Ni jambo la kawaida kujitokeza kwa lawama baada ya kufungwa na Bayern Munich,” Perez aliuambia mtandao wa Cadena Cope mara baada ya kupata ushindi huo dhidi ya Sutton.


“Kwa upande wetu hatuoni kama kuna tatizo lakini hatuwezi kufahamu kilichopo akilini mwake,” aliongeza nyota huyo.

No comments