MAINA BAND KUREKODI UPYA NYIMBO ZAKE TATU

BENDI ya muziki wa dansi ya Maina Band iko mbioni kuzirekodi upya nyimbo zake tatu ambazo ni “Maina ni Mtanzania Halisi”, “Nalia na Dunia” na “Rukia Wangu”, imefahamika.

Bosi wa Maina Band, Liston Maina ameiambia Saluti5 kuwa wameamua kuzirekodi upya nyimbo hizo kutokana na kutoridhishwa na ubora wake.

“Tumetazama ubora wa nyimbo hizo tukaona kuwa hauendani na soko la muziki la sasa hapa nchini na ndipo tunapanga kuzirudia upya ambapo pia tutaziongezea vionjo,” amesema Maina.


Amesema kuwa bado hawajapanga siku ya kuingia Studio ila amefafanua zaidi kwamba watakapokuwa tayari watazirekodi kwenye Studio za Amoroso, jijini Dar es Salaam.

No comments