MAINA BAND KUUNGURUMA MASTERS CLUB MIKOCHENI LEO

MAINA Band inayokusanya mastaa kibao wa muziki wa dansi, leo Jumapili kama kawaida itarindima Masters Club, Mikocheni jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 usiku na kuendelea hadi majogoo.

Bosi wa Maina Band ‘Wazee wa Cha Mwisho Raha’, Liston Maina ameitonya Saluti5 kuwa, watatumbuiza ndani ya Masters Club wanakopatikana kila wiki katika siku za Jumamosi na Jumapili, ambapo ameahidi burudani ya kukata na shoka.

“Kama kawaida ya bendi yetu, tutaangusha bonge la shoo litakalomudu vilivyo kumaliza kiu ya mashabiki wetu wa Mikocheni, hivyo tunawaomba wafike kwa wingi kupata kitu murua mioyoni mwao,” amesema Maina.


Baadhi ya mastaa wa muziki wa dansi wanaounda kikosi cha maina Band, ni pamoja na mwenyewe, Liston Maina, Fred Siame, Juma Membe, Papii Malay na Modwe Lubaba.

No comments