MAJERUHI SANTI CAZORLA AMNYONG'ONYESHA ARSENE WENGER

BOSI wa washika mitutu wa London, Arsene Wenger amesikitishwa na hatua ya kuumia kwa kiungo wake mahiri, santi Cazorla kwa kubainisha kuwa ni pigo kubwa kwa timu yake kwa sasa.

Akinukuliwa, Wenger alisema Cazorla ni kati ya wachezaji muhimu katika kikosi cha kwanza, hivyo kuumia kwake kutapunguza aina ya uchezaji wake na ni pengo.

“Kumkosa mtu kama Santi Cazorla ni pengo katika kikosi cha kwanza lakini sina jinsi kwasababu ni jambo lisilozuilika.”
“Nitaangalia namna ya kupanga kikosi bila ya kiungo wangu huyo na hili nalifanya kwa sababu ya kutaka kuendelea kuwa na kikosi cha kupambana ndani ya premier.”

Alisisitiza Wenger akinukuliwa na Sky Sports juu ya kuumia kwa kiungo huyo ambaye ni moja ya muhimili wa timu kwa sasa.

Santi Cazorla atalazimika kuwa nje ya uwanja kwa kipindi chote kilichosalia cha msimu huu kutokana na jeraha la kifundo cha mguu.

Cazorla hajacheza hadi alipochechemea na kuondoka uwanjani mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Ludogorets uwanjani Emirates mwezi Oktoba.

Alifanyiwa upasuaji mwezi Desemba na meneja wa The Gunners, Arsene Wenger alitumai mchezaji huyo wa miaka 32, angerejea kabla ya msimu huu kumalizika.


Lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania sasa ataangazia kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao.

No comments