MAMADOU ATHIBITISHA ALIHAHA KUTUA CRYSTAL PALACE

KWA siku mbili za mwisho za kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya, beki wa Liverpool, Mamadou Sakho alikuwa katika wakati mgumu zaidi.

Sakho na wakala wake wlisema zaidi kwa sababu ya kuvizia kuwahi kusajiliwa katika klabu ya Crystal Palace.

Wakala wake amesema kwamba kuna wakati walikuwa wamelazamika kuhamia katika ofisi ya mtendaji mkuu wa Liverpool  ambaye naye alikuwa mshirika mkubwa katika jambo hilo.

Mchezaji huyo raia wa Ufaransa hakuwa katika kiwango bora katika klabu yake tangu kutua kwa kocha raia wa Ujerumani Jurgen Klopp na hakucheza hata mechi moja msimu huu.

Na kocha wa Palace, Sam Allardyce alikuwa akisema kwamba kikosi chake kinamuhitaji Sakho kutokana na mapungufu ya nafasi yake katika ulinzi.

Hata hivyo Liverpool imekuwa klabu ambayo haiwaruhusu wachezaji wake kwa bei ya kitoto na imekuwa ikisema wazi kwamba kila mchezaji ambaye anauzwa na klabu hiyo hauzwi kwa bei ya hasara.

“Tofauti na timu nyingine sisi tunauza wachezaji kwa bei ya faida, tunawanunua kwingine waje hapa wang’are wakishindwa tunarudisha pesa yetu sio tunafanya kama sadaka,” amesema Klopp.

No comments