MASHABIKI, WADAU WAMSUBIRI KWA HAMU MSANII DARASA MWAKA 2017

PENGINE kinachosubiriwa hivi sasa katika medani ya muziki wa Kizazi Kipya ni kuona kama moto aliofungia nao mwaka 2016 msanii Darasa utaendelea mwaka huu, 2017 au la.

Wadau na mashabiki wa burudani wameonekana kupagawishwa vilivyo na kazi ya Darasa aliyoitoa mwishoni mwa mwaka uliopita kiasi kwamba ameumaliza kwa kuwapoteza kabisa mkali wa sauti na bingwa wa utunzi, Ali Kiba pamoja na msanii mwenye mafanikio zaidi kwa sasa Bongo, Diamond Platnumz.


Bila shaka kwa sasa kinachosubiriwa ni kuona kama je mwaka 2017 Darasa aliyefunga mwaka kwa kuwaloga kwa kibao kikali cha “Muziki”, ataendelea kutamba zaidi?

No comments