MASHAUZI CLASSIC YAPIGA HODI ‘USHUANI’ …Jumatano hii watakuwepo Next Door MasakiKundi la Mashauzi Classic chini ya Jike la Simba Isha Mashauzi, Jumatano hii litapiga hodi kwa washua wa Masaki jijini Dar es Salaam.

Mashauzi Classic watatumbuiza katika onyesho la “Usiku wa Marashi ya Pwani” litakalofanyika ndani ya klabu ya Next Door.

Mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Mashauzi ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo litakuwa la aina yake na kutakuwa na vikorombwezo kibao vya mambo ya pwani.

No comments