MATONYA KUFANYA REMIX YA WIMBO "ANITA" NA LADY JAYDEE

MKONGWE wa muziki wa Kizazi Kipya, Matonya amepanga kumsaka mkongwe mwenzake Lady Jaydee kwa lengo la kufanya nae remix ya wimbo wake uitwao “Anita” ambao aliwahi kutamba nao miaka ya nyuma.

Alisema kuwa kufanya remix ya wimbo huo inawezekana na kwamba kilichobaki ni yeye (Matonya) kumtafuta mwanadada huyo ili waangalie jinsi ya kufanikisha mpango huo.

“Kwa upande wangu hilo linawezekana kabisa, kilichobaki sasa ni kumtafuta Jaydee kwa lengo la kupata ukubali wake ili kazi ifanyike haraka iwezekanavyo,” alisema matonya kupitia mtandao wa Instagram.

Matonya alisema hayo wakati akijibu swali la mmoja wa mashabiki wake ambaye aliuliza kama msanii huyo ana mpango wa kufanya remix ya wimbo huo ambao amekiri kwamba ulimwingizia kiasi kikubwa cha fedha.   

No comments