MAURICIO POCHETTINO AMVULIA KOFIA VICTOR WANYAMA

MENEJA wa klabu ya Tottenham Hotspur, Mourcio Pochettino amemvulia kofia kiungo wa kati wa klabu hiyo kutoka Kenya, Victor Wanyama kwa kusema yuko katika kiwango kikubwa na ataisaidia timu msimu huu.

Kisha akabainisha kuwa uwezo anaouonyesha anajihakikishia namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza.

Akinukuliwa na BBC, kocha huyo alisema, mchezaji huyo ana sifa ya nguvu na uwezo wa kuisaidia sana klabu hiyo.

“Wanyama ninamfahamu vyema kwa sababu nilimnunua nikiwa Southampton kutoka Celtic. Ni rahisi sana kutambua sifa hizi,” alisema.

Meneja huyo alikuwa akijibu maswali kuhusu umuhimu wa mchezaji huyo kwenye klabu hiyo katika kikao na wanahabari katika kituo cha mafunzo cha klabu hiyo London.

Pochettino raia wa Argentina, alijiunga na Spur Mei, 2014 kwa mkataba wa miaka mitano na Mei, mwaka huu aliongeza mkataba huo na kuahidi kusalia White Hart Lane hadi 2021.

Wanyama alitua Spur kwa dau la pauni mil 11 akitokea Southampton katika dirisha la mwezi Juni, mwaka jana.


Kabla ya kuhamia Celtic, Mkenya huyo alikuwa anachezea Germain Beerschot ya Ubelgiji.

No comments