Habari

MECHI 6 BILA KUFUNGA BAO LOLOTE YAPELEKEA KUTIMULIWA KWA CLAUDIO RANIERI LEICESTER CITY

on

Leicester City imemtimua kocha wake Claudio Ranieri Alhamisi usiku ikiwa ni miezi tisa tangu awape taji la Premier League. 
Hilo lilikuwa taji la kwanza la Ligi Kuu katika historia ya klabu hiyo, lakini hiyo haijawazuia wamiliki wa timu hiyo inayopambana na vita vya kushuka daraja, kumtimua kocha. 
Hatua hiyo imekuja kuja siku chache baada ya wamiliki wa Leicester City kumkikingia kifua kocha huyo na kusema kibarua chake kiko salama.
Lakini baada ya kipigo kutoka kwa Seville katika Champions League ambacho kilichokuja baada ya michezo sita ya Premier League bila kufunga goli lolote, Ranieri akatimuliwa King Power Stadium. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *