MESUT OZIL AKANUSHA KUMKIMBIA ARSENE WENGER

MESUT Ozil amekuwa akihusishwa na taarifa za kutaka kuihama Arsenal kama hatua ya kupinga kuendelea kuwepo kwa bosi wake Arsene Wenger na tetesi zilisema kuwa uamuzi huo angeufanya katika kipindi cha usajili wa majira ya joto.

Lakini taarifa mpya zinasema kuwa Ozil amekanusha uvumi huo akisisitiza kuwa hana mpango wa kuikacha klabu hiyo na kwamba ana imani na kocha Arsene Wenger.

“Nimeshuhudia magazeti yakiandika mambo ambayo siyo kweli kuhusu mimi na kocha Arsene Wenger kwamba hatuna mahusiano mazuri na kwamba nimekerwa na kutotwaa mataji.”

“Hizi si taarifa za kweli hata kidogo kwa sababu ninaamini juu ya Arsene Wenger kwani ndiye aliyekuwa chanzo cha mimi kuja hapa Emirates, hili ni jambo lisiloweza kubadilika kata kidogo.”

“Ninawezaje kumkimbia Wenger ilihali ni mtu muhimu kwangu, ninachoweza kusema kuhusu uvumi huu ni kwamba mimi bado nitaendelea kukipiga Arsenal kwa nguvu zangu zote," alikiri Ozil.

Hata hivyo Ozil amekiri kuwa bado hajakubali kusaini kandarasi mpya kubaki Emirates ambao anahudumu mpaka mwishoni mwa mwaka 2018.


Ozil aliyejiunga na Arsenal mwaka 2013 akitokea Real Madrid kwa dau la pauni mil 42.5 amevumishwa kutaka kujiunga na Barcelona kwa dau la pauni mil 45.

No comments