Habari

MESUT OZIL SASA AGOMBANIWA NA BARCELONA, MANCHESTER CITY

on

TIMU ya Barcelona sasa inaongeza kasi ya kupata saini ya nyota wa washika
mitutu wa jijini London, Arsenal, Mesut Ozil.
Pamoja na Barcelona, pia matajiri wa jiji la Manchester, Manchester City
nao wameingia katika mbio za kumwania Ozil.
Hata hivyo, Ozil mwenyewe ameonyesha dhamira ya dhati ya kutotaka kuongeza
mkataba ndani ya arsenal na pia kuna tetesi kuwa kocha wa Manchester City, Pep
Guardiola ameonyesha azma ya kumwania.
Hata hivyo, taarifa za ndani ya The Gunners zinasema kuwa wanahitaji
kumwongezea kandarasi inayoweza kuishia mwishoni mwa msimu wa mwaka 2022 juu ya
mkataba wake wa sasa.

Uongozi wa Arsenal unahaha kuwaongezea mkataba mrefu wanandinga wawili
ambao ni Mesut Ozil na Alexis Sanchez ambao mikataba yao inamalizika mwishoni
mwa msimu wa mwaka 2018

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *