MIAKA 10 YA JAHAZI MODERN TAARAB KURINDIMA DAR LIVE JUMAMOSI HII


Hatimaye ile siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa taarab, imewadia ambapo kesho Jumamosi Jahazi Modern Taarab watafanya onyesho kubwa la kusherehekea miaka 10 ya uhai wa  kundi lao.

Onyesho hilo litafanyika ndani ya ukumbi wa Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam huku wasanii kadhaa waliowahi kuitumikia Jahazi miaka ya nyuma, wanatarajiwa kulipendezesha onyesho hilo.

Miongoni mwa wasanii waliothibitisha kushiriki onyesho hilo, ni pamoja na mwimbaji mkongwe Bi Mwanahawa Ali ambaye alitesa na nyimbo mbili ndani ya Jahazi “Roho Mbaya Haijengi” na “Wema Hazina Kwa Mungu” zilizotoka mwaka 2010 na 2011.

Jahazi inasherehekea miaka 10 huku malkia Leyla Rashid akiwa ndiye msanii pekee mwasisi wa bendi hiyo aliyebakia kundini.

Kundi hilo linatarajiwa kutumbuiza nyimbo zao zote kali kuanzia albam ya kwanza “Two in One” hadi “Kaning’ang’ania” bila kusahau vigongo vipya vya albam ijayo.

Super Shine Modern Taarab na Msagasumu ni miongoni mwa wasindikizaji wa show hiyo ya miaka 10 ya Jahazi Modern Taarab ndani ya Dar Live.

No comments