MJEDA ATUPWA JELA NIGERIA KWA KUMSHAMBULIA MSANII WA FILAMU

OFISA mmoja wa jeshi la Wananchi wa Nigeria, Suleiman Olamilekan amehukumiwa kutumikia jela kwa siku 28 na kufanyishwa kazi ngumu kwa kumshambulia msanii wa filamu.

Mwanajeshi huyo amebainika kuwa alimshambulia mwigizaji wa kike wa Nollywood, Ebere Ohakwe na baada ya kifungo hicho anaweza kuchukuliwa hatua zaidi ya kinidhamu.

Msemaji wa Jeshi, Kanali Aminu Iliyasu amesema jeshi halitamvumilia ofisa wake yeyote atakayebainika kuwanyanyasa raia kwa sababu zozote zile, kwani jukumu lao ni kuwalinda raia.

No comments