MKALI RONALDINHO AREJEA FC BARCELONA “KIBOSIBOSI”

MWANASOKA nyota wa zamani, Ronaldinho amepewa kazi katika klabu yake ya zamani ya Barcelona.

Straika huyo wa zamani wa Brazil ameteuliwa kuwa balozi maalum wa klabu hiyo ya Hispania.

Ronaldinho aliichezea Barcelona kati ya mwaka 2003 na 2008 na kuipa mafanikio makubwa klabu hiyo.


“Mara zote hata kabla ya kupewa wadhifa huu nilikuwa najihesabu mwakilishi mzuri wa Barcelona,” alisema Ronaldinho juzi.

No comments