MKHITARYAN, IBRAHIMOVIC, MARTIAL WAFANYA SIKU ZA WAYNE ROONEY MAN UNITED KUHESABIKA

SIKU za mshambuliaji Wayne Rooney kuwa ndani ya kikosi cha Manchester United zinaonekana kuhesabika.

Ujio wa Mkhitaryan, Zlatan Ibrahimovic na Anthony Martial unaiweka nafasi ya Rooney mashakani katika timu hiyo.

Umri wa Rooney umeenda na kiwango kimeshuka nah ii inamfanya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha United.

Rooney ameshawahi sana kuhusishwa kuondoka Man United , haijaanza leo kwa Rooney kuhusishwa na uhamisho wa kuondoka United.

Ikumbukwe msimu wa mwisho wa Sir Alex Ferguson Wayne Rooney alihusishwa na uhamisho wa kwenda Chelsea japo jambo hilo halikutokea.

Lakini sasa tetesi za Rooney kuondoka Man United zimepamba moto sana. Wakati wa dirisha dogo la usajili wa Januari kuliibuka tetesi za Wayne kuhamia Ligi ya China.

Japokuwa klabu ambayo ilikuwa ikihitaji huduma ya Wayne Rooney haikutajwa kwa kipindi hicho, ila ilikuwa wazi kwamba Wayne angevutwa China kutokana na nguvu kubwa ya kifedha ya nchi hiyo.

Tianjin Quanjian, timu inayonolewa na nahodha wa zamani wa Italia, Fabio Cannavaro imekiri kuwahi kufanya mazungumzo na Rooney.

Cannavaro amekiri walimuhitaji Rooney japokuwa hafiti katika staili yake ya uchezaji ila walijaribu kutaka kumsajili Wayne Rooney.


Tianjin Quanjian bado inapewa nafasi kubwa ya kumnunua Rooney, japokuwa wanasema katika mipango yao ya usajili jina la mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre Aubemayang ndio liko juu.

No comments