MKONGWE ROGER MILLA AMPONGEZA KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON

KOCHA wa timu ya taifa ya Cameroon “Indomitable Lions”, Hugo Broos raia wa Ubelgiji amefagiliwa kwa kuifanya timu hiyo kucheza kitimu licha ya kuwa na muda mfupi wa kuiandaa.

Kocha huyo amewaduwaza wengi kwa kuiwezesha Cameroon kutinga fainali ya afrika nchini Gaborn, licha ya kwamba hakufikisha hata mwaka mmoja tangu ateuliwe kuinoa.

Cameroon ilionyesha soka la hali ya juu ilipomenyana na Senegal na baadae kuitoa Ghana 2-0 katika nusu fainali.


Nguli wa soka wa Cameroon, Roger Milla alisema kocha huyo amefanya kazi kubwa na nzuri ukilinganisha na kocha aliyetimuliwa, Volker Finke raia wa Ujerumani.

No comments