MKUU WA MKOA NJOMBE ATOA ZAWADI YA UWANJA WA KISASA WA SOKA

KUTOKANA na furaha ya timu ya Mji Njombe kupanda daraja, mkuu wa mkoa huo, Christopher Ole-Sendeka ameahidi kujenga uwanja wa kisasa wa soka.

Akizungumza wakati wa kuwapokea mashujaa hao waliorejea kifua mbele baada ya kuhitimisha mechi za mwisho za Ligi Daraja la Kwanza na kuongoza Kundi hivyo kutangazwa kupanda daraja, Ole-Sendeka alisema ni lazima mkoa ufanye jambo kuonyesha kuguswa.

Alisema, kitu pekee wanachoweza kukifanya na kikawa cha maana ni kujenga uwanja wa kisasa wa soka ambao utatumiwa na timu hiyo pamoja na nyingine.

“Katika kuenzi mchango wa vijana hawa na kuonyesha tunaunga mkono michezo kwa dhati, mimi nitakaa na Katibu Tawala, mkurugenzi, wahandisi, watendaji wote na wataalamu kuangalia namna ya kufanikisha hili,” alisema.


Mbali ya Njombe Mji, timu nyingine zilizofanikiwa kupanda daraja ni Lipuli ya Iringa na Singida United ya Singida.

No comments