MO MUSIC AHOFIA KUGEUZWA "ATM" KUJIINGIZA KWENYE MAHUSIANO YA MAPENZI

MO Music amesema kuwa hataki kujitosa kwenye mahusiano ya kimapenzi akihofia kugeuzwa ATM kwa madai kuwa baadhi ya wasichana wanawapenda wasanii kwa sababu ya fedha.

“Wengi wanakupenda kama Mo Music na sio mimi kama. Wanawake wengi sasa hivi wanaangalia watu wenye kitu, ingawa sio wote ila asilimia kubwa,” alisema Mo Music.

Alisema kuwa tabia hiyo ndio inamfanya ajiepushe na mambo ya mahusiano ili kulinda kile anachokipata kwa ajili ya maisha yake badala ya kuendekeza vitu ambavyo havina faida.


Msanii huyo ambaye anatamba na kibao chake kipya kiitwacho “Adoado” alisema kuwa bado anaishi kivyake huku akiangalia mtu makini ambaye atamchukua na kuishi nae kuliko kuvamia na kujikuta akichunwa kile anachopata katika kipato chake.

No comments