MOURINHO AIPA ‘NDOO’ YA KWANZA MANCHESTER UNITED EFL CUP …Southampton yalala 3-2, Ibrahimovic shujaa


Manchester United imetwaa taji la kwanza wakiwa chini ya kocha Jose Mourinho  baada ya kuilamba Southampton 3-2 katika mchezo mkali wa fainali ya EFL Cup.

Katika mchezo huo uliochewa kwenye dimba la Wembley, United ilikuwa ikiongoza 2-0 hadi jirani na mapumziko kwa mabao ya Zlatan Ibrahimovic (dakika ya 19) na Jesse Lingard (dakika ya 38), lakini Southampton wakapunguza moja kwa bao la dakika ya 45 kupitia kwa Manolo Gabbiadini.

Ilipotimu dakika ya 48, Manolo Gabbiadini akachanua tena kwa kuisawazishia Southampton na kuufanya mchezo uwe wa mshike mshike mkubwa.


Wakati ikiaminika kuwa mchezo utaenda hatua ya dakika 30 za nyongeza, Ibrahimovic akaifungia Manchester United bao la ushindi dakika ya 87.

Manchester Utd (4-2-3-1): de Gea 6.5, Valencia 6, Bailly 5.5, Smalling 5.5, Rojo 5, Ander Herrera 7.5, Pogba 5.5, Lingard 7.5 (Rashford 77), Mata 6 (Carrick 46, 6), Martial 5.5 (Fellaini 90), Ibrahimovic 8.5. 

Southampton (4-3-3): Forster 6, Cedric 6, Stephens 6, Yoshida 6, Bertrand 6, Ward-Prowse 7, Romeu 7, Davis 6 (Rodriguez 90), Redmond 7.5, Gabbiadini 8 (Long 83 6), Tadic 6 (Boufal 77). 

No comments