MOURINHO AIPONGEZA CHELSEA NA KUITAKA IANGALIE KOMBE LA FA

KOCHA wa Manchester United Jose Mourinho amesema klabu ya Chelsea inaweza kuangazia michuano ya Kombe la FA kwani tayari wanajua ni mabingwa wa Ligi Kuu England.

Vijana hao wa Antonio Conte ambao watawakaribisha Man United Stamford Bridge katika robo fainali Kombe la FA mwezi Machi wako mbele kwa alama nane katika msimamo wa Ligi na bado wamesalia na michezo 13.

Chelsea waliendelea na makali yao kwa kuendelea kuichapa Woltes 2-0 katika raundi ya tano ya Kombe la FA huku United wakitoka nyuma kwa kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Blackurn.

“Kombe la FA ni kitu muhimu sana kwao,” amesema meneja huyo wa zamani wa Blues.

Msimamo wa Ligi ya EPL 2016/17 Chelsea wanapigiwa upatu kushinda Ligi kwa mara ya pili kwa miaka mitatu baada ya Mourinho kuhama na kutwaa ubingwa akiwa nao msimu wa 2014/15.

“Chelsea wanaweza kuangazia vyema michuano mingine inayowatatiza. Kombe la FA ni muhimu kwao.”

Katika msimu wa kwanza wa meneja Mourinho uwanjani Old Trafford amepongeza klabu hiyo kuwa miongoni mwa timu 32 bora katika Ligi ya Europa ambapo kwa sasa wamo kifua mbele kwa magoli 3-0 dhidi ya saint-Etienneya Ufaransa.


United wanashikilia nafasi ya sita katika jedwali la Ligi ya Premier.

No comments