MOURINHO ASHUSHA PRESHA YA WAYNE ROONEY MANCHESTER UNITED

KOCHA wa Manchester United Mreno Jeso Mourinho ameshusha presha ya naodha wake Wayne Rooney kwa kumwaambia bado anaaminika ndani ya kikosi cha sasa.

Hatua hii imemfanya Rooney awe na uhakika wa kuendelea kuvaa kitambaa cha unaodha wa mashetani hao wa jiji la Manchester United.

Hii inatokana na ukweli kuwa hatima ya Rooney ilikuwa mashakani kwani kocha Jose Mourinho alionyesha nia ya kutokumwamini katika kikosi cha kwanza lakini Mourinho ametamka wazi kuwa nahodha huyo bado ni mtu muhimu ndani ya kikosi na kwamba hayumo katika mpango wa kumruhusu aondoke ndani ya Old Trafford.


Kocha huyo amesema kwamba kwa kawaida mchezaji anakuwa bora zaidi kadri anapokuwa ana miaka mingi ndani ya kikosi kama alivyo Rooney.

No comments