MOURINHO: NILIGOMEA OFA YA FEDHA NYINGI KWENDA KUFUNDISHA SOKA CHINA

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amefichua siri kuwa aligomea ofa ya fedha nyingi kwenda kufundisha soka China.

Mourinho alisema alichukua uamuzi huo kwa kutafakari kuwa alikuwa anajiona ana umri mdogo kwenda kufundisha soka nchini humo.

Alisema hata hivyo haikuwa na maana alikuwa anaponda watu wanaotaka kwenda kujiunga na klabu za huko ambazo zimekuwa zikimwaga mamilioni ya fedha katika siku za karibuni.


Mourinho alisema, amesikia baadhi ya makocha wanaoponda watu wa soka wanaokwenda china, lakini yeye haoni tatizo.

No comments