MOUSSA DEMBELE ACHEKELEA KUENDELEA NA SOKA LA CELTIC

MOUSSA Dembele amesema ana furaha kuendelea na soka ndani ya Celtic, licha ya Chelsea kuwa kwenye rada za kuwania saini yake kipindi cha dirisha dogo mwezi uliopita.

Dembele, 20, alifunga hat-trick timu yake ilipoibuka na ushindi wa 5-2 baada ya kupona majeraha.

Chelsea iliripotiwa kutaka kumsajili Dembele kwa pauni mil 40.

“Nina furaha kujifunza hapa ndio maana nimesaini tena.”
“Najifunza kwenye moja ya klabu kubwa, nina furaha.”
Dembele ambaye alikosa michezo miwili, alifunga mabao 23 kwenye Ligi ya Scotland.

Tetesi kwa Dembele alikuwa akihitajika na Chelsea zilivuja alipoonekana anapanda ndege kwenda London siku ya mwisho kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa Januari 31, mwaka huu.

Celtic ilisisitiza kwamba mchezaji huyo alikuwa akisafiri kwenda kumuona mtaalamu wa goti linalomsumbua.
Mtaalamu huyo wa goti anapatikana jirani na Stanford Bridge yalipo makao ya Chelsea.


Celtic haikupata ofa kutoka katika klabu yoyote inayoshiriki Ligi Kuu England.

No comments