MWAMUZI JANNY SIKAWE AMIMINIWA SIFA NA KAMATI YA WAAMUZI AFRIKA

KAMATI ya waamuzi barani Afrika imemfagilia mwamuzi kutoka nchini Zambia, Janny Sikazwe ikisema yuko katika kiwango cha juu cha uchezeshaji kwa sasa.

Mwamuzi huyo ndiye aliyepewa kuchezesha fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika iliyopigwa jana ikiwakutanisha Cameroon na Misri.

Sikazwe mwenye miaka 37, aliwahi kutwaa tuzo ya mwamuzi bora wa mwaka wa CAF 2015.

Katika michuano ya mwaka huu alichezesha vyema pambano gumu la majirani na mahasimu wa kisoka kati ya Cameroon na Burkina Faso katika hatua ya makundi, ambalo lilimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Aidha alisemama katika kuchezesha mchezo war obo fainali kati ya Cameroon “Indomitable Lions” na Senegal ambapo mshindi alipatikana kwa matuta5-4.


Mwamuzi huyo mwenye begi la Shirikisho la soka la kimataifa, huo ulikuwa mchezo wake wa pili mkubwa wa fainali kwani mwaka 2016 alichezesha fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia kati ya Real Madrid na Kashima Antlers.

No comments