MWIGIZAJI NOLLYWOOD AMSHUKIA RAIS MUHAMAD BUHARI… asema ameshindwa kuongoza nchi

MWIGIZAJI mahiri wa kike wa filamu za Nollywood, Funke Adesiyan amemshukia rais Muhamadu Buhari akisema ameshindwa kuongoza nchi.

Achana na kushindwa kutimiza ahadi yake ya kuwarejesha wasichana na Chibok waliotekwa na wanamgambo wa Boko Haram, Fuke anasema rais ameshindwa katika mambo mengi.

“Rais Buhari ameitumbukiza nchi kwenye lindi la umasikini, ananifanya nijipongeze kwa kutompa kura yangu, kwa hakika anaipeleka nchi pabaya,” alisema.


Mrembo huyo ameandika kwenye mtandao wake wa Instagram akisema anaamini rais huyo asipobadilika, wananchi wa Nigeria watamchoka hata kabla ya kumaliza muhula wake wa kwanza madarakani.

No comments