NAY WA MITEGO ADAI KANISA LAKE HALITAKUWA NA SADAKA

NAY wa Mitego anasema anafungua kanisa lake la kumuabudu Mungu ambapo amedai kuwa kanisa lake litakuwa si la biashara bali ni la kumuabudu Mwenyezi Mungu aliye hai.

“Acha kanisa likamilike, Mwenyezi Mungu anisimamie tutajua nini kinaenda kutokea lakini sio kanisa kwa ajili ya kupiga hela,” Nay aliiambia eNews.

Nay amedai kuwa mchungaji wa kanisa lake atakuwa tofauti na hatotegemea sadaka za waumini ili kuendesha maisha yake bali kazi zake nyingine ndizo zitakazoweza kumwingizia kipato.

Rapa huyo amejinadi kuwa anatarajia kupata waumini wengi kupitia kanisa lake na kwamba litakuwa chanzo cha mafanikio katika mambo yao.


Nay amedai kuwa kanisa lake litajengwa Mbezi ya Kimara jijini Dar es Salaam.

No comments