NEVILLE AMSHAURI ROONEY KUACHANA NA HABARI ZA KUTAKA KUTIMKIA CHINA

STAA wa zamani Phil Neville amemshauri mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney kuelekeza nguvu katika kikosi hicho badala ya kufikiria kwenda kucheza soka la kulipwa nchini China.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya England ameshindwa kupata nafasi ya kucheza muda mwingi chini ya kocha Jose Mourinho na kwamba kwa sasa kuna klabu kadhaa nchini China ambazo zinamuhitaji.

Mapema wiki hii pia Mourinho alisema kuwa wala hafahamu kama rooney atabaki kwenye klabu hiyo lakini akasema hatamlazimisha nyota kuondoka.

Kutokana na hali hiyo Neville alisema juzi kuwa anavyoamini Rooney bado anaweza kutoa mchango mkubwa kwa Man United msimu huu na kwamba rekodi yake ya upachikaji mabao inaweza kumfanya ang’are katika mechi ya fainali ya Kombe la IFL dhidi ya Southampton, hususan baada ya mpinzani wake, Henrikh Mkhitaryan kuumia katika mchezo ambao Man United waliondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sant Etienne katika michuano ya Ligi ya Europe.  


Akizungumza juzi kiungo huyo wa zamani wa Man United katika mahojiano na kipindi cha BBC 5 Live Sport, alisema kuwa sio kwamba anampa ushauri lakini anachoweza kusema ni kuwa staa huyo anatakiwa kuelekeza nguvu zake kuitumikia Manchester United.

No comments