NEYMAR KUSIMAMA KIZIMBANI BAADA YA RUFAA YAKE KUTUPILIWA MBALI

STRAIKA wa Barcelona, Neymar JR aanatarajia kusimama kizimbani nchini Hispania kwa tuhuma za rushwa baada ya kupoteza rufaa iliyopinga madai hayo.

Hatua hiyo imekuja baada ya mahakama kuu nchini humo kukataa rufaa hiyo.

Taarifa zinaeleza kuwa mbali na rufaa ya staa huyo pia na iliyokatwa na klabu yake ya Barcelona na ya klabu yake ya zamani ya Santos na ya kampuni inayoendeshwa na baba yake vilevile zimekataliwa.

Mashitaka ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 25, yanahusu uhamisho wake wa kujiunga na klabu hiyo ya Camp Nou akitokea Santos mwaka 2013, ambapo waendesha mastaka wa nchini Brazil wanadai kuwa kiasi kinachotajwa ni kidogo.


Kutokana na hali hiyo waendesha mashitaka wanataka Neymar na baba yake waende jela miaka miwili lakini kutokana na kuwa ni kosa lao la kwanza hawataweza kwenda ndani.

No comments